ZA UKWELI SANA

Kampuni ya Tigo yaanza kusaidia Miradi ya kijamii Zanzibar.

kampuni ya mtandao wa simu tigo imesema itaanza kusaidiana na zanzibar kwa kuwekeza zaidi kwenye masuala ya mawasiliano na pia kuanza kusaidia kwenye masuala ya kijaamii.Akizungumza na makamu wa Raisi wapili wa Zanzibar balozi seif Alli Idd,Bwana Arthur Basting makamu wa Raisi wa kampuni ya Tigo yenye makao yake makuu Stokholmes Sweden amesema kuwa amefurahishwa sana kuona kwamba tigo imeenea Africa nzima.
  Naye Bi Sylivia Bwalire meneja uendeshaji wa tigo hapa Tanzania amesema tigo imejipanga vema kushirikiana na Zanzibar kwenye uwekezaji Masuala ya mitandao na huduma za kijamii Unguja na Pemba,Balozi seif Alli Idd aliwashukuru tigo kwa hatua hiyo amesema itasaidia sana kwani hata School nyingi nchini humo hazina vikalio.

       pichani makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif All idd,akizungumza na makamu wa Rais wa tigo ndugu Arthur Basting na meneja uendeshaji wa tigo hapa nchini Bi sylivia Bwalire

0 Response to "Kampuni ya Tigo yaanza kusaidia Miradi ya kijamii Zanzibar."

Chapisha Maoni