ZA UKWELI SANA

MUNGU YUPO NAWE SIKU ZOTE.

   Mpendwa msomaji wa makala hii kupitia blogu yako pendwa,habari ya jumatatu tulivu kabisa wengi hupenda kuiita blue Monday,lakini mimi huiita jumatatu njema na mpya kwako,pole na uchovu na hekaheka za weekend nzima,ni matumaini yangu kwamba upo salama salmini kiafya huku joto la uchaguzi likiwa limezidi kupanda kiasi lakini sio vibaya pia kwa leo tukakumbushana mambo ya msingi kidogo,''unajua maisha ni safari yenye milima na mabonde,kuna wakati wa kupata na mara nyingine pia kuna wakati wakukosa,kuna wakati wa furaha na wakati wa huzuni pia,napenda kukumbusha nyakati zote hizo Mungu Mwenye enzi pia  bado yupo na anatenda kazi zake maishani mwako kama kawaida na kamwe hajakuacha wala hajakusahau kabisa,Mungu yupo pamoja nawe unachopaswa kufahamu ni kwamba kila jambo linalotokea chini ya jua liwe  baya au zuri yeye ndiye huruhusu matokeo yote hayo,na wakati mwingine matatizo au changamoto za kimaisha huruhusiwa na Mungu zitokee ili kutuimarisha zaidi na kutukumbusha kwamba yeye Mungu Mwenye Enzi yupo na kwamba tusitegemee akili zetu wenyewe kwa kila jambo hapa duniani''
      Mungu yupo anataka wanadamu tumkumbuke yeye na tumwamini kwa kila jambo,kwa hiyo tunachopaswa  kufanya tupatapo magumu ni kupiga magoti na kumshukuru MUNGU kisha tumwombe atupitishe salama katika wakati huo mgumu,kwani tukiweka tumaini la kweli na tukavuta taswira na kuweka fikra za kushinda basi tutashinda tu kinachofanya tusifanikiwe ni kwamba jamii ya leo,wengi hatumwamini MUNGU bali tunamwogopa tu tukisikia habari zake,tunaamini anaweza kutuletea mabaya zaidi ya mazuri inafikia mahala mtu akifanikiwa kidogo utasikia watu wakisema ''huyu amejiunga na freemason'' sasa hatuamini kwamba mungu anaweza kumfanikishia mwadamu maisha yake isipokuwa shetani tu,hili kwa kweli si sawa hembu tubadilishe namna ya  kufikiri  tufikiri chanya zaidi kwa kila jambo na tumpe mungu tumaini la maisha yetu
  ndugu  msomaji siko hapa kuhubiri dini ila napenda watu wa imani zote waelewe kwamba mungu ni msaada mkubwa sana katika maisha yetu lakini imani yako na ukaribu na MUNGU ndio utakaofanikisha maisha yako kwa kila jambo unaliliomba,,ndiyo maana mtaalamu mmoja wa mambo ya imani anasema,kwa kila kitu utakachokiomba kwa mfano kama Unaamini katika mizimu,majabali au masanamu kama ukiamini kiukweli na kuvuta picha kama umefanikiwa basi utafanikiwa tu,kwani MUNGU anafanya kazi kupitia fikra na mawazo yako mwenyewe.kwa hiyo kama mawazo yako yapo kwenye uwoga na kushindwa utashindwa  tu lakini kama unawaza kufanikiwa basi mungu anatumia taswira unayovuta katika mawazo yako,na fikra na atakupatia ushindi kwa hiyo jitahidi  kila mara uwazapo uwaze mawazo mazuri tu,kwani kila wazo utakalowaza litahesabika kuwa ni maombi kwa mungu.


      NAWATAKIENI JUMATATU NJEMA.
PIGA 0656538476 KWA MATUMIZI YA OFISI TU PIA USISITE KUTUTUMIA MAONI YAKO.

0 Response to "MUNGU YUPO NAWE SIKU ZOTE."

Chapisha Maoni