ZA UKWELI SANA

HUU NDIO UKWELI WA SOKO LA FILAMU BONGO KWA SASA.





miaka kadhaa nyuma soko la filamu za kihindi lilishika sana kasi hapa nyumbani wabongo wengi walipenda sana kuzitazama,kwenye vibanda umiza na  hata majumbani mwao,msimu huo ulidumu kwa muda mrefu hatimaye ukapita ukaja msimu wa filamu za kinigeria,pia ulidumu sana kwa muda mrefu hatimaye ukapita,na mungu si athumani wala abdala wabongo wakaamka toka usingizini na wakaanza kutengeneza filamu zao wenyewe japo kwa hali ngumu kidogo waliweza kujitoa katika michezo ya kuigiza katika radio na televisheni na walianza kutengeneza filamu zao za kwanza mwanzoni mwa miaka ya 2005 walitengeneza filamu za mwanzoni  nyingi japo nyingine hazikuweza kutoka,na zilizotoka hazikupata umaarufu sana kama filamu iliyofanywa na marehemu kanumba na ray the greatest kama anavyojiita na johari chagula wakishirikiana na waigizaji wengine wakongwe kwa kipindi hicho,huo ulikuwa mwanzo mzuri sana baada ya hapo ray na kanumba waliweza kutoa filamu kali siku hadi siku na soko la filamu likakuwa zaidi,hapa bongo na watu walianza kupenda filamu zao za nyumbani,wasanii waliongezeka na ajira pia zikaongezeka sana,japo changamoto za hapa na pale hazikukosekana.

     Baaada ya mungu kumpenda zaidi marehemu kanumba,watu wengi wamekuwa wakilalamika kuyumba sana kwa soko la filamu hapa nchini,huku wadau wakitaja sababu nyingi zinazosababisha changamoto hiyo kuwepo.Jumanne hii katika kipindi cha take one,cha clouds tv kinachoongozwa na mtangazaji wa kipindi hicho aitwaye zamaradi mketema,alihojiwa vincent kigosi ray na  aunt Ezekieli,ray alipoulizwa kuhusu swali la kuyumba kwa filamu amesema kuwa sio kwamba soko limeshuka bali siku hizi hakuna ushindani kwani yeye na kanumba walikuwa na ushindani wa kimaendeleo,kanumba akienda kuchukua vifaa marekani yeye anakwenda china,ila kwa sasa hakuna ushindani huo wa kimaendeleo,pia amesema kwamba suala la uwizi wa kazi zao maarufu kama piracy linawasumbua sana kwani sokoni kazi original haziuziki zinanunuliwa zaidi kazi feki,na hivyo wasanii kutonufaika na kazi zao kabisa,hivyo wasanii wadogo wanaumia zaidi kwani hakuna wanacho nufaika zaidi ya maproducer wakubwa japo ray the great amesema kwake yeye hali sio mbaya ameweza kununua magari mazuri na kujenga  hata nyumba,hizo ni sababu za wasanii lakini kwa uchunguzi tulioufanya tumebaini kwamba maproducer wakubwa hawawapi nafasi wasanii chipukizi,yaani wanabania vipaji vipya kila siku sura ni zilezile na hivyo kupoteza mvuto machoni mwa watazamaji na ubunifu kupungua sana kwani maproducer  wa filamu wanaangalia sura na sio uwezo wa msanii hivyo wasanii hupewa hata nafasi wasizo zimudu hali inayopelekea kuidumaza zaidi tasnia ya filamu hapa nchini.Marehemu steven kanumba alijaribu kutambulisha sura mpya nyingi sana kwenye tasnia kama irene uwoya,irene paul,wakina jenifa na wengineo kanumba hakuwa mchoyo aliwapatia fursa na watu wengine kitu ambacho kwa sasa kimepotea sana.
wadau mnapaswa kusimama kila mmoja kwa nafasi yake kutetea soko la filamu bongo,kwani ndio sekta iliyoajiri vijana wengi zaidi,serikali wanapaswa pia kuchukua hatua za haraka kurekebisha hiyo hali na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
0656538476.

0 Response to "HUU NDIO UKWELI WA SOKO LA FILAMU BONGO KWA SASA."

Chapisha Maoni