ZA UKWELI SANA

NI YA KIJANA ALIYEZAMIA KWENYE TAIRI ZA NDEGE HUKO NIGERIA.

moja ya stori zilizokuwa kubwa sana miaka ya nyuma,ilikuwa ni watu mbalimbali hasa vijana kufanya uzamiaji kwa njia ya meli,inafahamika kama stowaway kwa lengo la kwenda nchi za ulaya,marekani,afrika kusini na nyinginezo,vijana waliokuwa wakifanya hivi ni kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.

Hii imesikika sana nchi za kaskazini mwa afrika,Tunisia ikiwa ni mojawapo ambapo kumekuwa na wazamiaji wakielekea ulaya kutafuta maisha mazuri,lakini kutoka uwanja wa ndege wa murtala Muhammed,Lagos Nigeria,kijana mdogo amekutwa akiwa amejificha ndani ya sehemu zinakoingia tairi za ndege moja ya kukodi iliyokuwa uwanjani hapo.

Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege la Tag Aviation ilikuwa imeegeshwa huku marubani wakifanya ukaguzi kabla ya kuiwasha engine ndipo walipomkuta kijana huyo akiwa na simu mbili za mkononi ambazo hazikuwa na laini.

amesema kuwa alifanikiwa kuingia sehemu hiyo kwa kusaidiwa na kaka yake.

DOGO HUYO KATIKA PICHA UWANJANI HAPO.

0 Response to "NI YA KIJANA ALIYEZAMIA KWENYE TAIRI ZA NDEGE HUKO NIGERIA."

Chapisha Maoni