ZA UKWELI SANA

CHUKI, FITINA NA MAJUNGU KIKWAZO KIKUU CHA MAENDELEO.

mpenzi msomaji wa blogu hii pendwa kabisa kwa vijana,habari za muda na wakati kama huu,pia pole sana na majukumu ya kila siku katika ujenzi wa taifa letu,leo mungu amenijalia kuniletea ujumbe huu mzito ambao naamini utakapo maliza kusoma makala hii utakuwa umejengeka na kubadilisha mtazamo wako na namna nzuri kabisa ya kufikiri.


kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza,suala la chuki,fitina na majungu si geni masikioni mwako,labda imekutokea wewe kuchukiwa na watu,kwa sababu fulani aidha za msingi au zisizo za maana,au wewe umeshawahi kumchukia mtu kwa namna moja au nyingine,kimsingi suala la chuki halijengi kabisa kwani licha ya athari ya kutokuwa na umoja na kuleta mabadiliko chanya katika jamii,pia kubeba chuki na visasi huweza kusababisha magonjwa,kama presha,vidonda vya tumbo na mengine yanayofanana na hayo.
kumekuwa na mfululizo wa chuki binafsi,majungu na fitna maeneo mengi kama mashuleni,maofisi na maeneo mengi tu ya jumuiya yanayofanana na hayo,japo leo nisingependa kuzungumzia huko sana bali ningependa kugusia kuhusu tasnia zetu za sanaa bongo kama bongo muvi,na muziki wa kizazi kipya,hivi karibuni kumekuwa na vurugu nyingi kwenye show wanazofanya Diamond na Ally kiba,mashabiki wa wanamuziki hao wawili,wamekuwa wakisababisha uvunjifu wa amani kwenye kumbi za burudani kila jamaa hawa wawili wanapokutana,hatukatai ushabiki au ushindani wa muziki hapana.
suala la ushindani lipo hata ulaya,lakini kwa hapa bongo imekuwa ni chuki kiasi hata cha mastaa wetu hawa wakubwa kushindwa hata kusalimiana,hii ni mbaya sana wakati wenzetu wa nigeria,wakipeana sapoti katika mziki wao,na kupigwa tafu hata na serikali yao sisi huku,tunachukiana na kutupiana lawama zisizokuwa na misingi ambazo zingeweza kutatuliwa tu na waungwana bila kufika mbali na kuwa makubwa,hii ni aibu kwa taifa ambalo mziki wake unakuwa kwa kasi na kuleta sifa kwa taifa,na kufunguwa fursa kubwa ya ajira kwa vijana.
mbaya zaidi kama si nzuri sana,muziki sasa hivi umekuwa na mashabiki bongo kama simba na yanga,kwa kweli nyinyi wasanii wenyewe mkionyesha na kukiri,mbele za vyombo vya habari kwamba hamna maelewano mnaleta mgawanyiko na kutokuelawana hata kwa mashabiki zenu,kilichotokea kwenye tamasha la tigo mapema mwezi uliopita si kitendo kizuri kabisa,kwani mashabiki waliovalia tshirt za team ally kiba,walimzomea mwanamuziki diamond na kumtupia chupa na makopo akiwa jukwaani,kitendo kilicho mfanya awarushie pesa mashabiki hao kwa hesabu za haraka haraka kama takribani milioni moja na nusu zilimtoka pale,haikuwa busara sana kwani wengi wa mashabiki wale vipato vyao ni vya chini sana,kwa hiyo unapotoa noti ya shilingi elfu kumi na kuirusha hewani maana yake unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na hata vifo,japokuwa jambo la kumshukuru mungu hakuna baya lililotokea mahala pale.







wakati tukiwa katika msimu huu wa valentine day,wawapendanao tunawashauri mashabiki na wasanii wote wapendane chuki hazijengi,na dawa ya kufanikiwa ni kufanya jambo kwa jitihada na sio chuki aliyepewa kapewa tu,tukubali changamoto bila changamoto hakuna mafanikio,wabongo tumezowea majungu na chuki,nakumbuka hata marehemu kanumba,alikashifiwa na kudharauliwa sana alipokuwa hai,lakini alipokufa alipata sifa kibao sana,diamond amelita heshima na kutambulika kwa taifa,amefika ambapo hatukuwahi kufika hata ukubali au ukatae Diamond is the best,sambaza upendo sio chuki na majungu.


nakutakia valentine day njema
tuwasiliane hapa 0656538476.






0 Response to "CHUKI, FITINA NA MAJUNGU KIKWAZO KIKUU CHA MAENDELEO."

Chapisha Maoni