ZA UKWELI SANA

ADHABU WALIZOPEWA MORIS NA OKWI .

Wiki mbili zilizopita katika mechi 2 za ligi kuu,kulitokea matukio mawili ambayo yalileta mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini.
mchezaji wa azam fc,aggrey moris alimpiga kiwiko emannuel okwi katika mechi iliyowakutanisha simba vs.mtibwa,kitendo kilichopelekea okwi kuzimia uwanjani na kupelekwa hospitali kitendo kingine kilikuwa kikimuhusisha mchezaji wa mbeya city juma nyoso ambaye alionekana akimshika makalio mchezaji wa simba Elias Maguri.

Baada ya mjadala mkubwa kwenye mitandao na magazeti hatimaye jana kamati, ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania limewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji juma nyoso wa mbeya city na Aggrey Moris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyo yafanya wakiwa uwanjani.
Nyoso alilamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa simba amefungiwa mechi nane za ligi kuu ya vodacom ,akiwa mbele ya kamati hiyo jana february 6,alikiri kufanya kitendo hicho na kumuomba radhi Maguri.

Naye Moris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga kiwiko OKWI wakati timu hizo zilipokuwa kwenye mechi ya ligi iliyochezwa january mwaka huu,uwanja wa taifa Dar,

0 Response to "ADHABU WALIZOPEWA MORIS NA OKWI ."

Chapisha Maoni