ZA UKWELI SANA

MREMBO ALILIA MILIONI TANO ILI AWE KAMA ZAMANI

Msichana Zuhura juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar,ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75 na kumsababishia maumivu makali,anahitaji kiasi cha shilingi 5,000,000 ili aweze kufanyiwa upasuaji nchini India. Msichana Zuhura Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha kilo 75. Uvimbe huo unaomfanya alie kila mara ulifanya kampuni ya Global publishers kushirikiana na kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na kituo cha tv cha dtv,kuwasiliana na daktari aitwaye Sabapathy wa India aliyekubali kuifanya kazi hiyo kwa kiwango hicho cha cha fedha tofauti na madai ya awali kuwa zingehitajika millioni 30. Daktari huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo kama hayo ambaye hali yake inaendelea vyema,alisema msichana huyo atarejea katika hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini kwake na kumpangia tarehe ya upasuaji hapo Oktoba 25 mwaka huu. Zuhura amewaomba watanzania kumsaidia ili kuweza kupata matibabu hayo aweze kupona na kuendelea kuwasaidia watoto wake ambao ni wadogo wanahitaji msaada wake kama mama na kwamba anayeguswa na tatizo linalomkabili anaweza kumsaidia kupitia namba yake 0717319555. by Global publishers.

0 Response to "MREMBO ALILIA MILIONI TANO ILI AWE KAMA ZAMANI"

Chapisha Maoni