ZA UKWELI SANA

LADY HANIFA MBARONI KWA KUTAKA KUUA

Rb namba WH/RB/6335/2014 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI kwenye kituo cha polisi cha Wazo Hill,Tegeta jijini Dar,imemtia mbaroni mtangazaji maarufu bongo aitwaye Hanifa Hamidu "Lady Hanifa na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu wa baa aliyetambulika kwa jina la Aika Endrew(32) Uchunguzi ulibaini tukio hilo limetokea wiki iliyopita katika baa maarufu ya shayo iliyopo maeneo ya Tegeta jijini Dar Siku ya tukio hilo Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo nakuketi ndipo akaja Aika na kumkumbusha deni lake la bia moja aliyokopa jana,lakini hali hiyo lady hakuifurahia na kuona kwamba amefedheheshwa,ndipo alipo kwenda jikoni kuangalia biashara yake na kumuita mfanyakazi wake anaye itwa Aneth ili ampatie hela yake,ndipo alipoanza kudai chenji yake kwa mabavu hapo ndipo utata ulipoanzia na ndipo Lady Hanifa alimchoma mlalamikaji kisu mkononi na tumboni,na Aneth kumsaidia Hanifa kumchoma mlalamikaji kwa upawa wa kuchomea Chipsi Shingoni na kumjeruhi vibaya mno,Hanifa na Aneth walikimbia polisi Haraka ndipo baadae mlalamikaji akiwa amesindikizwa na watu wengine walifika kituoni hapo na kutoa maelezo ndipo Aneth na Lady Hanifa wakashikiliwa na polisi kituoni hapo Wazo Hill.mtangazaji maarufu bongo lady Hanifa.

0 Response to "LADY HANIFA MBARONI KWA KUTAKA KUUA"

Chapisha Maoni