ZA UKWELI SANA

MBONGO BADILISHA FIKRA,TUSIMWAGE DAMU ZA NDUGU ZETU.

Nilikuwa nafikiria sana kuhusu makundi yanayojiita ya msimamo mkali ya dini kama BOKO HARAM,na ISLAMIC STATE,yanayo sifika kwa kuuwa na kuteka watu kwa madai ya kueneza dini na Kutetea dini yao na wamemwaga damu za watu wengi sana,huku wakijitapa kwenye television kubwa duniani kwamba wataendeleza mchezo wao.


hilo likiendelea huko kwa wenzetu huku kwetu,tumeanza kuiga tabia hizo na kuwatukana wenzetu wa imani nyingine hadharani bila uwoga huku viongozi wa imani moja wakiwashambulia wengine na kuwaaigiza waumini wao wasishirikiane na watu wa imani nyingine.Jamani waafrika tuwe makini na mafundisho ya kigeni ambayo yatavuruga amani ya nchi yetu,uislamu na ukristo ni dini tulizoletewa sisi tulikuwa na dini za mababu zetu,tuwaachie wenyewe upuuzi wao sisi tuige yaliyomema.

0 Response to "MBONGO BADILISHA FIKRA,TUSIMWAGE DAMU ZA NDUGU ZETU."

Chapisha Maoni