ZA UKWELI SANA

Albino walia kilio cha samaki Machozi kwenda na Maji

   Hivi karibuni kumeripotiwa kuibuka upya kwa mauaji ya kinyama ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) ambayo yalipotea kwa muda,ambapo kwa mara ya kwanza mauaji haya kusikika kwa nguvu ilikuwa mnamo mwaka 2005.
  Mauaji hayo hayo yalizimika kwa muda na kuibuka tena mwa 2010 na sasa mwaka huu tena ambapo kwa mwaka huu unyama huo uliweza kutokea kwenye kijiji cha Bunokela Igunga mkoani Tabora ambapo wauaji hao walivamia nyumba ya Mashiri Masaga na kumkata mikono mke wa ndugu Masaga,kwa jina Mungu Masaga na kumkata mikono yake yote miwili na kumua mumewe bwana Mashiri Masaga katika harakati za kumtetea mke wake.
   Mnamo mwaka 2010 huko Bukoba wauaji hao walimvamia Mariam Stanford nyumbani kwao na kumkata pia mikono yake yote miwili licha ya Mariam kumuona kwa macho jirani yake bwana John Jonsoni mahakama ilisema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa.
    Kumekuwa na maneno mengi juu ya mauaji haya ya albino,wengine wakidai viungo vya albino hasa mwanamke vina bahati sana kwa hivyo kama unavipata kwenye shughuli za uchimbaji madini utaweza kuwa milionea kwa kupata madini mengi sana,Swali mbona Albino wao wenyewe ni masikini kupita kiasi?
    Maneno mengine ni kwamba kuna uvumi wanasiasa huvitumia viungo vya ndugu zetu kupata mvuto wa kisiasa na hili likihusishwa sana na vipindi matukio haya yakitokea ni karibia na uchaguzi mwaka 2005,2010,na huu 2014 kuelekea uchaguzi mkuu.
      Serikali imefanya jitihada za kila namna kukabiliana na mauaji haya lakini inaonekana kuzidiwa nguvu kwani mauaji haya huibuka kila kukicha,na kumekuwa hakuna adhabu ya kueleweka na kuadabisha kwa wale wanaopatikana na hatia hali inayotupa mashaka na serikali yetu kwamba iko makini na hili swala?
   Hivi majuzi alinukuliwa Mkurugenzi wa makampuni ya Ipp Dkt Reginald Mengi akisema atatoa kiasi cha pesa kwa mtu atakaye taja watu wanao jihusisha na mauaji haya.Lakini mbunge wa viti maalumu anayewakilisha watu wenye ulemavu bungeni bi Alyshaima kwegir alisema anawaomba watu wenye uwezo kama Dkt Mengi wangesaidia kuwatoa huko vijijini kwani nyumba za wahanga wengi ziko mbalimbali sana kiasi cha kilometa 100 hadi 200 ndio ukute nyumba nyingine hali inayofanya majangili hao kutekeleza azma zao kiurahisi sana kwani hata mhanga apige kelele ni ngumu kufikiwana msaada kwa haraka sana aliyasema hayo mbunge huyo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha asubuhi cha Clouds tv 360 kinachorushwa na clouds tv.
    Pia Alyshaima alisema jeshi la polisi linafanya kazi katika kukabiliana na unyama huo lakini linakabiliwa na changamoto nyingi kama vile usafiri magari machache na mabovu,nyumba mbovu na ukosefu wa posho au motisha hali inayowafanya kufanya kazi kwa kusuasua.
  Alipoulizwa kwanini serikali sasa isifanye jambo hili seriously zaidi kwa kuanzisha oparesheni kama zile za tokomeza ujangili na operesheni kimbunga zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa alisema wazo hilo lipo na mwezi desemba watapeleka muswada huo bungeni.
   Mtanzania mwenzangu wauaji hawa tunao kwenye jamii na ni ndugu zetu tusiiachie tu serikali tutoe elimu zaidi kwa jamii zetu na tutoe taarifa polisi kuwafichua wauaji hao.
     Habari na picha na yusuph Hamisi Mbuguni.

0 Response to "Albino walia kilio cha samaki Machozi kwenda na Maji"

Chapisha Maoni